Picha kwa hisani –
Tume ya uwiano na utangamano wa taifa NCIC imewaonya wanasiasa wanaoendeleza kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge wa Msambweni dhidi wa kuendeleza siasa za mgawanyiko.
Akizingumza na Wanahabari katika eneo la Ng’ombeni kaunti ya Kwale, Kamishna wa Tume hiyo Philip Okundi amesema tayari tume ya NCIC imeweka maafisa maalum wa kuchunguza wanasiasa hao.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tume hiyo Millicent Okach amewasihi vijana kutokubali kutumiwa na wanasiasa, na badala yake kuungana na viongozi walio na sera za kufanikisha maendeleo.