Picha kwa hisani –
Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC, imeidhinisha mswada wa BBI wa mwaka wa 2020 uliowasilisha na wale wanaounga mkono hali inayopelekea mchakato wa kuifanyia marekebisho Katiba kuendelea.
Tume ya IEBC inayoongozwa na Mwenyekiti Wafula Chebukati, imesema imeidhinisha mswada huo baada ya kukagua saini milioni 4.2 na kuidhinisha saini milioni 1.4 zilizokuwa sahihi.
IEBC, imesema tayari imewaandikia barua maspika wote katika kaunti zote 47 nchini inayopendekeza mabunge ya kaunti kushuhulikia mswada huo na kuwasilisha ripoti zao kwa bunge la Seneti na lile la kitaifa kwa kipindi cha miezi mitatu ijayo.
Hata hivyo kupita kwa mswada huo na kupelekea wakenya kushiriki zoezi la kura ya maamuzi kunahitaji mabunge ya kaunti 24 kuunga mkono mswada huo kabla ya kuuwasilisha mbele ya bunge ya Seneti na lile la kitaifa.