Chama cha waalimu wa shule za upili na vyuo vya kadri nchini KUPPET kimezidi kuishinikiza tume ya kuajiri waalimu nchini TSC kuhakikisha waalimu ambao hawajasajiliwa na tume hiyo hawafundishi katika shule za humu nchini.
Katibu wa chama hicho kaunti ya kwale Mackenzie John Tuki amesema hatua hiyo itasaidia kuimarisha viwango vya elimu akidai kwamba idadi kubwa ya walimu wanaofundisha humu nchini hawajahitimu.
Hata hivyo ameitaka Tume ya TSC kuajiri walimu zaidi kwani idadi kubwa ya wakenya wamesomea taaluma hiyo lakini hawajapata ajira.
Taarifa na Hussein Mdune.