Picha kwa hisani –
Tume ya kuajiri waalimu nchini TSC imewaagiza waalimu wa shule za msingi na upili kote nchini kurejea kazini ifikapo siku ya jumatatu jumalijalo, ili kuendeleza matayarisho ya kufunguliwa shule za humu nchini.
Akizungumza katika makao makuu ya taasisis ya KICD baada ya kikao cha wadao wa elimu kupanga mikakati ya kufunguliwa kwa shule,afisa mkuu mtendaji wa tume hio Nancy Macharia amesema waalimu watahakikisha wanafunzi wanaendeleza masomo kufidia muda walioupoteza wakiwa nyumbani.
Macharia aidha amesema waalimu wako huru kurejea shule kuanzia hii leo hadi siku ya jumatatu juma lijalo ili wapate muda wa kijiandaa kikamilifu kwa ajili ya kurejelea masomo.
Kwa upande wake waziri wa elimu nchini Prof George Magoha amesema watafanya mkutano mwengine wa wadau wa elimu kabla siku ya jumatatu juma lijalo na wataidhinisha mapendekezo rasmi ya kufunguliwa shule za humu nchini.