Picha kwa hisani –
Rais wa Marekani Donald Trump amesema ataondoka katika Ikulu White House ikiwa Rais mteule Joe Biden atadhinishwa rasmi kuwa rais wa taifa hilo kwa kura za wajumbe zilizopigwa Novemba 3.
Trump ameshinikilia msimamo wake kuwa uchaguzi mkuu wa urais nchini humo ulikumbwa na udanganyifu licha ya Biden kuonekana kuongoza kura za wajumbe kwa kupata kura 306 huku Trump akiwa na kura 232.
Wawakilishi wa kura za wajumbe watakutana mapema Januari mwaka ujao kuidhinisha rasmi kura zilizopigwa huku rais mteule Joe Biden wa chama cha Democratic, akisubiri kuapishwa kuwa rais Januari 20.