Story by Janet Shume-
Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC imemtangaza Issa Abdhallah Timamy kama gavana wa kaunti ya Lamu baada ya kuibuka mshindi.
Timamy imemshinda mpinzani wake wa karibu Fahim Twaha aliyekuwa gavana wa kaunti hiyo kuanzia mwaka 2017-2022.
Akizungumza baada ya kupokea cheti chake kutoka kwa IEBC, Timamy ameahidi kuweka kipau mbele suala la maendeleo katika kaunti hiyo ili kuboresha maisha ya wakaazi.
Hata hivyo maafisa wa IEBC kaunti ya Lamu wamelalamikia idadi ndogo ya wakaazi waliojitokeza kupiga kura katika uchaguzi wa Agosti 9, wakiwahimiza viongozi wa eneo hilo kuendeleza hamasa kwa wakaazi kuhusu umuhimu wa upigaji kura.