Taarifa Gabriel Mwaganjoni
Aliyekuwa katibu wa Serikali ya Kaunti ya Mombasa Francis Thoya ameitaka Serikali kuzindua upya shughuli za kusafisha na kusafirisha mafuta ya petroli zilizokuwa zikiendelezwa katika eneo la Changamwe kaunti ya Mombasa.
Thoya amesema kiwanda cha ‘Kenya Petroleum Refineries Limited’ katika eneo la Changamwe kilitekeleza majukumu makubwa ya kulikuza taifa hili kiuchumi na kufungwa kwake hakujaleta manufaa yoyote kwa wakaazi wa Mombasa.
Akizungumza na Wanahabari, Thoya amesema kaunti ya Mombasa itasambaratika kiuchumi ikiwa viwanda kama hivyo vitafungwa licha ya kuwa tegemeo kubwa la ukuaji wa uchumi.
Kiwanda hicho kwa sasa kinatumika kama hifadhi ya mafuta pekee huku asilimia 50 ya shughuli za usafishaji na usafirishaji wa mafuta ya petroli kutoka Bandari ya Mombasa zikisalia kufungwa kwa takriban miaka 10 sasa.