Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.
Ili kuboresha huduma za serikali kwa wakaazi wa maeneo ya Samburu, Taru na Macknon Road katika gatuzi dogo la Kinango, sasa Tarafa ya Samburu imebadilishwa na kuwa Gatuzi dogo.
Mshirikishi mkuu wa utawala kanda ya Pwani John Elungata, amesema eneo la Samburu linakabiliwa na changamoto nyingi na linastahili kuwa na Naibu kamishna ili asimamie shughuli na mahitaji msingi ya Wakaazi wa eneo hilo.
Elungata amehoji kwamba huduma ikiwemo vitambulisho vya kitaifa, vyeti vya kuzaliwa na huduma nyingine msingi zitakuwa zikitolewa katika eneo hilo la Samburu kama Gatuzi dogo.