Story by Hussein Mdune-
Mbunge wa Matuga Kassim Tandaza amewataka viongozi wanagombea nyadhfa mbalimbali za uongozi eneo hilo kukoma kueneza siasa za propaganda.
Akiongea kwenye mikutano yake ya kisiasa Tandaza amesema kuna baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaoeneza siasa za migawanyiko, akiwataka kukoma mara moja limegawanyika mara mbili hatua ambayo.
Tandaza amesema msimu huu wa siasa viongozi hao wanafaa kueneza sera za za maendeleo kwa wananchi na wala sio siasa za chuki na migawanyiko.
Hata hivyo amewataka wakaazi wa Matuga kudumisha amani sawa na kuwachagua viongozi ambao wataleta maendeleo.