Mbunge wa Matuga Kassim Sawa Tandaza ameonya kuwachukuliwa hatua kali za kisheria baadhi ya wazazi wanaokosa kufikisha shuleni fedha za basari na badala yake kuzitumia fedha hizo kwa malengo yao binafsi.
Tandaza amesema kwa ushirikiano na vitengo vya usalama wataanza uchunguzi kuhusiana na swala hilo kwani ni makosa makubwa kwa mzazi yeyote yule kubadili jina la mtoto la basari na kujiandisha mwenye ili kutumia fedha hizo.
Akizungumza na Wanahabari baada ya kupeana hundi ya shilingi milioni 7 kwa wanafunzi 464 wa vyuo vikuu na taasisi za mafunzo, Tandaza amesema viwango vya elimu katika eneo bunge la Matuga vimeimarika kutokana na ushirikiano wa wadau wote.
Kwa upande wao wazazi ambao watoto wao wamenufainaka na fedha hizo akiwemo Samwel Chikophe Mwero amesema fedha hizo zitawasaidia pakubwa wanafunzi kimasomo.