Story by Our Correspondents-
Mbunge wa Matuga Kassim Sawa Tandaza ameanzisha ujenzi wa jengo la ghorofa katika shule ya msingi ya Kwale litakalotumika kama madarasa ya shule hiyo ili kuendeleza elimu.
Akizungumza na Wanahabari baada ya kuweka jiwe la msingi katika shule hiyo, Tandaza ameweka wazi kwa ujenzi wa jengo hilo jipya utagharimu kima cha shilingi milioni 10.
Tandaza amesema makubaliano walioafikiana na mwanakandarasi yaliyepewa zabuni ya ujenzi wa jengo hilo katika shuleni hiyo ya msingi ya Kwale anatarajiwa kukamilisha ujenzi huo mwezi Disemba mwaka huu.
Wakati uo huo amedokeza kwamba barabara kuu ya Kwale-Kinango tayari imekabidhiwa mwanakandarasi na hivi karibuni barabara hiyo itaanza kuwekwa lami ili kurahisisha shughuli za uchukizi katika barabara hiyo.