Story by Salim Mwakazi-
Mbunge wa Matuga Kassim Sawa Tandaza ameilaumu serikali ya kitaifa kwa kushindwa kutatua mizozo ya ardhi inayoshuhudiwa katika eneo bunge hilo.
Akizungumza katika eneo la Mkokoni, Tandaza amesema mizozo ya ardhi katika kaunti nzima ya Kwale inatokana na hatua ya serikali kuzifanya ardhi hizo kuwa ardhi za jamii.
Kiongozi huyo amesema hatua hiyo imechangia kuongezeka kwa mizozo ya ardhi baina ya wenyeji na mabwenyenye wanaonyakua ardhi hizo.
Wakati uo huo amedokeza kwamba tayari amewasilisha hoja bungeni itakayochangia wakaazi wa eneo bunge hilo wanapata haki.