
Mbunge wa Matuga, Kassim Sawa Tandaza
Mbunge wa Matuga, Kassim Sawa Tandaza amesema kuwepo na vituo vya kurekebisha walanguzi wa mihadarati hakutachangia kumaliza suala la mihadarati.
Kwa mazungumzo ya kipekee na mwandishi wetu mjini Mombasa Tandaza amesema endapo vituo hivyo vitakuwa vikiendelea kuhudumu basi ulanguzi wa mihadarati hauta koma hapa Pwani.
Wakati uo huo amevitaka vitengo vya usalama kushika doria kikamilifu nchi kavu na majini ili kuhakikisha hakuna namna ambayo mihadarati inafikia watumizi.