Picha Kwa Hisani
Wiki moja baada ya Loveness Malinzi maarufu kama ‘Diva The Boss’ kusema kwamba anampenda nyota wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, mwanamuziki kutoka Kenya Tanasha Donna amevujisha picha inayomuonesha akiwa na msanii huyo kwenye treni na kusindikiza na ujumbe ambao uliibua mjadala mitandaoni.
Ujumbe huo ulisoma hivi, “Unbreakable.” Shughuli ya wambeya kwenye mtandao wa Instagram ikawa ni kutaka kujua picha hiyo ilichukuliwa wapi na lini.
“Hii ni wapi tena jamani mbona sielewi haya mapichapicha,” alichangia mdau mmoja mtandaoni.
Mjadala huo ulizidi kuwa mkubwa ambapo watu wengi walichukua picha hiyo na kuisambaza kwenye kurasa mbalimbali hususan zile ambazo zinadili na umbeya.
“Amkeni amkeni, achana na Diva ambaye yeye alimchimba kidogo Zari ambaye kwa sasa inaonekana yupo mambo yao si mchezo huko Sauz, Tanasha naye kaachia hii mbona wanatuchanganya hawa watu,” alichangia mdau mwingine mwenye ushawishi kwa umbeya mjini Instagram.
Diva naye amekuwa akikesha akimsifia Diamond kwenye ukurasa wake wa Instagram. Ikumbukwe kwamba, Diva na Diamond au Mondi hawakuwa na uhusiano mzuri kwa miaka mingi kiasi cha chuki kutamalaki kati yao.
Kwa kipindi chote, Diva alikuwa shabiki kindakindaki wa mkali wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ kabla ya kuhamia kwa Rajab Abdul ‘Harmonize’.Hata hivyo, kwa sasa Diva anasemekana kufika mbali zaidi kiasi cha kumchimba mzazi mwenza au baby mama wa Mondi, Zari.
Baada ya kipindi kirefu, hivi karibuni Diva alianza kufunguka kwamba yeye ni shabiki namba moja wa Mondi hadi hapo atakapoingia kaburini na yupo tayari kupambana na yeyote atakayekuwa kinyume na staa huyo wa Wimbo wa Waah.
Mbali na mapenzi, Diva anasema kuwa anamkubali sana Mondi kwani anafanya kazi kwa bidii na anaona ameleta mabadiliko kwenye muziki.