Picha kwa hisani –
Wafugaji wanaotafuta lishe la mifugo yao na maji katika kaunti ya Tana River wanapaswa kuomba ruhusa kutoka kwa wazee wa kaunti hiyo kabla ya kuwalisha mifugo yao.
Mshirikishi mkuu wa utawala kanda ya Pwani John Elungata amesema mara nyingi wafugaji hao wamekuwa wakiwalisha mifugo yao kwenye mashamba ya wenyeji, hali inayozua taharuki katika kaunti hiyo.
Akizungumza huko Tana River baada ya kuongoza misururu ya mikutano ya amani na usalama, Elungata amesema ni sharti wafugaji na wakulima katika Kaunti hiyo ya Tana River waheshimiane.
Wakati uo huo Elungata ameitaka kamati maalum ya wazee katika kila eneo la kaunti hiyo kuwajibika na kuhakikisha maswala ya amani na usalama yanapewa kipau mbele miongoni mwa jamii yao.