Taarifa na Alphalet Mwadime.
Shirika la kupambana na uraibu wa dawa za kulevya la Reachout Centre Trust limesema kuwa kaunti ya Mombasa ina takriban watu elfu 10 waliyoathirika na uraibu wa dawa za kulevya.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika hilo Taib Abdulrahman amesema kwamba hali hiyo inastahili kuangaziwa, ikiwemo wadau kushirikiana na serikali kujitokeza katika kuikabili.
Akihutubu katika uwanja wa Makadara Mjini Mombasa wakati wa maadhimisho ya siku ya kupambana na ulanguzi wa mihadarati ulimwenguni, Taib amedokeza kwamba watoto wa hadi umri wa miaka 12 wamejitosa katika uraibu wa dawa za kulevya katika Kaunti hiyo.
Kulingana na Taib tayari harakati za kuikabili hali hiyo zinaendelezwa japo zinahitaji kuungwa mkono kikamilifu na Serikali.