Story by Janet Shume –
Takriban wanafunzi 118 waliokuwa wakifadhiliwa na benki ya Equity kupitia mpango wa elimu wa Wings to fly ikiwemo wale waliofanya vyema katika mtihani wa kitaifa wa KCSE mwaka 2019 wamepokea ufadhili wa masomo ya vyuo vikuu.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Afisa mkuu mtendaji wa benki ya Equity Dkt James Mwangi amesema idadi hiyo ya wanafunzi iko juu mno ikilinganishwa na wale waliopata ufadhili mwaka wa 2020.
Dkt Mwangi amesema idadi hiyo imeonyesha wazi jinsi wanafunzi wa humu nchini wanavyojibidisha zaidi shuleni, akisema ufadhili wa masomo kwa wanafunzi utachangia wanafunzi kufanya vyema zaidi masomoni.
Hata hivyoiAkiitaja hatua hiyo kama itakayoimarisha viwango vya elimu nchini pamoja na kuimarisha maisha ya wakaazi.