Picha kwa hisani –
Takwimu kutoka kwa wizara ya afya katika kaunti ya Taita Taveta zimebainisha kwamba kaunti hio ina zaidi ya watu elfu moja wanaogua maradhi ya akili.
Akizungumza mjini Wundanyi,waziri wa afya katika serikali ya kaunti ya Taita Taveta John Mwakima amesema huenda idadi hiyo ikaongezeka iwapo wananchi hawatojitokeza kufanyiwa vipimo vya maradhi hayo.
Mwakima amehusisha ongezeko la visa vya maradhi ya akili miongoni mwa wakaazi na utumizi wa dawa za kulevya akiwataka vijana kujiepusha na utumizi wa dawa za kulevya na badala yake kujihusha na maswala ya maendeleo.