Picha kwa Hisani –
Serikali ya kaunti ya Taita – Taveta inaendeleza mazungumzo na serikali ya kitaifa ili kufufua huduma za reli katika kaunti hio.
Gavana wa Taita -Taveta Granton Samboja amesema mazungumzo hayo yamefikia hatua ya mwisho na kwamba kufufuliwa kwa reli eneo hilo kutaimarisha uchumi wa kaunti hio na taifa kwa jumla.
Samboja amesema mpango huo wa kufufua huduma za reli katika kaunti hio utakapofanikishwa utasaidia wakulima na wafanyibiashara kusafirisha bidhaa zao kwa urahisi.
Amesema kuidhinishwa kwa mradi huo kutasaidia miji mbali mbali ya kaunti hio ya Taita taveta kuimarika zaidi.