Picha kwa hisani –
Wizara ya Afya nchini imenakili visa vipya 1,253 vya maambukizi ya virusi vya Corona baada ya sampuli 10,170 kufanyiwa uchunguzi na idadi hiyo kufikia watu 86,383.
Akitangaza takwimu hizo, Katibu mkuu msimamizi katika Wizara hiyo Dkt Rashid Aman, amesema kenya imenakili idadi kubwa ya watu waliopona virusi hivyo 11,324 katika muda was aa 24 zilizopita na idadi hiyo kuongezeka hadi watu 67,788.
Dkt Aman amesema watu 16 wameripotiwa kuaga dunia katika mda wa saa 24 na kuchangia idadi hiyo kufikia watu 1500.
Akigusia swala la marufuku ya usafiri iliotolewa na taifa la Marekani dhidi ya raia wake wanaolenga kuzuru humu nchini, Dkt Aman amesema japo swala hilo sio zuri kwa uchumi wa nchini lakini kila taifa la mipango yake ya kuzuia virusi vya Corona.
Aidha amewahimiza wakenya kuzidi kuzingatia masharti ya kujikinga na virusi vya Corona ili kuzuia msambao wa virusi hivyo nchini.