Taarifa na Gabriel Mwaganjoni
Mombasa, Kenya, Oktoba 22 – Kuwashirikisha waraibu wa dawa za kulevya katika harakati mbalimbali za kujinasua ndio hatua ya kipekee inayoweza kuwakinga vijana wengi wa Kaunti ya Mombasa katika uraibu huo.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika linalopambana na uraibu wa dawa za kulevya miongoni mwa jamii la Reachout Centre Trust, Taib Abdulrahman amesema kuwahusisha waraibu hao katika vikao mbalimbali vya kijamii, kuwahamasisha kuhusu athari za dawa za kuelvya na kuwahusisha katika kazi za kijamii kumesaidia katika kuwaondoa kwenye janga hilo.
Akizungumza mjini Mombasa, Taib amefichua kwamba Shirika hilo linawekeza mbinu mbalimbali za kuhakikisha kwamba waraibu hao wanachukua jukumu wao wenyewe ili kujiondoa kwenye uraibu huo na kuwa watu muhimu wa kutegemewa katika jamii.