Story by Gabriel Mwaganjoni –
Huduma za kuwanasua waraibu wa dawa za kulevya zilizotekelewa wakati wa mwezi wa Ramadhan zilichangia mabadiliko makubwa katika kuwanasua vijana katika janamizi hilo.
Mkuruegzni mkuu wa Shirika la Reachout Centre Trust Taib Abdulrahman amesema huduma msingi ikiwemo kuwatibu waraibu hao na tiba ya Methadone, kumesaidia jamii kuwanusuru vijana wao kutoka kwa makali ya mihadarati.
Kulingana na Taib, hali ya waraibu hao kudumisha mfungo wa Ramadhan sawia na kutumia tiba ya Methadone ilijenga uiano na kuwasukuma karibu na Mwenyezi Mungu.
Mwanaharakati huyo hata hivyo amekiri kuwa mbinu ya kutoa mafunzo ya kidini sawa na kuishirikisha jamii katika makabiliano hayo imesaidia kuwashawishi vijana kuasi uraibu wa mihadarati.