Mke wa Ali Kiba adai talaka.
Picha Kwa Hisani.
Mke wa mwanamuziki nyota wa Tanzania Ali kiba, Amina Khalef amewasilisha kesi mahakamani ya kutaka kutengana mume wake.
Amina aliwasilisha kesi hiyo ya talaka katika mahakama ya Kadhi ya Mombasa mwezi jana baada ya miaka mitatu kwenye ndoa.
Picha Kwa Hisani.
Aidha, alieleza kuwa sababu kuu ya kuvunja ndoa yake na mwanamuziki huyo ni kuwa na msongo wa mawazo na kutelekezwa na mumewe huku akibaini kuwa Ali Kiba atekelezi majukumu kama mume.
Wawili hao walioana mwaka wa 2018, kwa sheria za Kiislamu ambapo kwa sherehe kubwa iliyoandaliwa jiji Mombasa huku mashabiki wakitaja harusi hio kuwa ya kupigiwa mfano.
Picha Kwa Hisani.
Ali Kiba amejiunga na watu mashahuri ambao wanatarajiwa kutalikiana na wake zao mwaka huu.