Taarifa na Sammy Kamande
Mombasa, Kenya, Juni 22 – Mwenyekiti wa bodi ya taasisi za mafunzo ya utabibu nchini Philip Kaloki, amesema bodi hiyo ina mipango ya kuhakikisha taasisi hizo zinaongezwa ili kutoa nafasi zaidi kwa wanafunzi wanaolenga kusomea taaluma ya udaktari.
Akizungumza kule mjini Mombasa wakati wa hafla ya kuwatuza walimu wa taasisi hizo, Kaloki amesema wanapania kuwa na madaktari sawia na wauguzi wa kutosha katika hospitali mbali mbali kote nchini.
Amesema baada ya kipindi cha miaka minne, bodi hiyo itakuwa imefanikisha mpango wa kuwa na madaktari wa kutosha katika hospitali zote za umma na zahanati za humu nchini.
Wakati uo huo amedai kuwa walimu wa taasisi hizo wanazidi kuwaelimisha wanafunzi wanaosomea taaluma hiyo ya udaktari ili kuhakikisha wanakuwa waadilifu.