Picha kwa hisani –
Taasisi ya utafiti wa matibabu nchini KEMRI inatarajiwa kuanzisha zoezi la kufanyia majaribio chanjo ya virusi vya corona hivi karibuni.
Mkurugenzi mkuu wa taasisi hio Profesa Yeri Kombe amesema tayari wamepata kibali kutoka kwa idara husika kitakacho wawezesha kutoa chanjo hio kwa wananchi.
Akizungumza baada ya kamati ya bunge la kitaifa kuhusu afya kufanya ziara katika taasisi hio,Kombe amesema majaribio hayo yatafanyiwa watu 40 watakaojitolea na hapo baadae chanjo hio itatolewa kwa zaidi ya watu miatatu.
Naye mwenyekiti wa kamati bunge la kitaifa kuhusu afya aliyezungumza wakati wa ziara hio Sabina Chege amesema watashinikiza serikali kufadhili kituo hicho ili kufanikisha shughuli zake.
Kufikia sasa zaidi ya watu 8,000 wamejitolea kupewa chanjo hio.