Mwenyekiti wa Tume ya kitaifa ya ardhi Mohamed Swazuri amewaongoza Makamishna wengine wa tume hiyo kutathmini ardhi zilizonyakuliwa katika eneo la Mama ngina kule mjini Mombasa.
Hatua ya Tume hiyo imejiri baada ya Rais Uhuru Kenyatta siku ya Jumatatu, kuiagiza tume hiyo kuzirudisha ardhi zote zilizonyakuliwa katika eneo la Mama ngina kwa serikali.
Akizungumza na Wanahabari, Swazur amesema kuwa jumla ya mabwenyenye 13 wanadai kumiliki vipande vya ardhi kwenye ardhi hiyo yenye ekari 26, wanamiliki vipande hivyo vya ardhi kinyume cha sheria kwani ardhi hiyo ni ya umma.
Swaziri pia ametoa makataa ya siku 90 kwa wale wote walionyakua ardhi katika eneo hilo kuzirudisha mara moja kwa serikali kabla ya tume hiyo kufuatilia mbali hati miliki za ardhi hizo.
Wakati uo uo amedokeza kuwa hati miliki hizo zitatupiliwa mbali na kuchapisha rasmi kutotambuliwa kwa hati miliki hizo kwenye gazeti la serikali hivi karibuni.
Taarifa na Radio Kaya.