Msaanii Susumila amefungika na kuelezea uhalisia wa uhusiano wake na Gavana wa kaunti ya Mombasa Ali Hassan Joho.
Akiongea na Uhondo mchana wa leo Susumila ameeleza kuwa wawili hao wamekuwa na uhusiano mzuri kwa muda wa miaka 12.
“Kile ambacho watu hawakijui kunihusu ni kuwa mimi na Gavana Joho tupo na uhusiano mzuri. Nimemjua kwa muda wa miaka 12 sasa. Ni kutokana na uhusiano huu ndio ameamua kunisaidia katika safari yangu ya mziki, Kwa sasa yeye ndiye amesimamia kazi yangu na Jolie,” amesema Susumila.
Kando na Susumila Gavana Joho ameonekana wazi wazi akimpa shavu msanii kutoka Tanzania kwa jina Ali Kiba. Hivi majuzi alinunua tiketi zote za Tamasha lake lilofanyika Mombasa.
Taarifa na Dominick Mwambui.