Msanii Susumila amekiri kuchoshwa na taifa lake, Kenya kufuatia ufisadi uliokithiri kwa sasa.
Msanii huyo ameleezea kutamausha na hatu ya kuvunjwa kwa majumba hali inayopelekea hasara kubwa kwa waekezaji.
‘Yani katika hii nchi kama kuna dhambi kubwa yenye madhara makubwa ni ufisadi yani naangalia yale majumba yanabomolewa naangalia investors wamepoteza mabilioni mangapi alafu naangalia watu wangapi wamepoteza ajira naangalia maisha ya watu wangapi yatatatizwa na hii story yote alafu najiuliza hawa wahusika walikua wapi ujenzi ukianza kuanzia msingi mpaka jengo linaigia watu na maduka na biashara tofautitofauti zinafanyika Kenya imenichosha lakini bora uhai,’ameandika msanii huyo.
Taarifa na Dominick Mwambui.