Msaidizi wa kaunti Kamishna eneo la Matuga, Denis Barassa amewataka wakaazi wa mazumalume wadi ya Tsimba/Golini kaunti ya Kwale kufanya kila juhudi kuhakikisha wanapata vyeti vya umiliki wa ardhi.
Akiongea huko Mazumalume wakati alipokutana na wakaazi wa eneo hilo kutafuta suluhu ya unyakuzi wa ardhi, Barasa amesema njia pekee ya kuwakomesha mabwenyenye kunyakuwa ardhi zao ni kuhakikisha kila mmiliki wa ardhi anapata hati miliki.
Barasa ametaja kuwa mkaazi akiwa na hati miliki ya ardhi, itamuwezesha kuishi katika maisha yalio huru na kufanya shughuli zake za kujiendeleza ikiwemo Kilimo katika ardhi zao.
Akigusia suala la ugatuzi, Barassa amewataka wakaazi hao kujua haki zao za kimsingi kwa kile alichokitaja kuwa wananchi wamekuwa wakinyanyaswa na viongozi ikiwemo kukosa kufaidika na miradi mbalimbal.
Taarifa na Mariam Gao.