Mwakilishi maalum kutoka Mombasa Fatuma Kushe amesema kuwa visa vya mimba za mapema hususani sehemu za mashinani vitapungua endapo walimu na wazazi watakuwa na ushirikiano bora.
Kulingana na Fatuma maeneo mengi katika kaunti za ukanda wa Pwani zimeathirika na visa hivyo na kupelekea na sekta ya elimu kubakia nyuma.
Aidha amesema tayari Ameanzisha mradi maalum wa kuhamasa wanafinzi wa kike shule mbali katika kaunti yabmombada kuhusu athari ya mimba za mapema.
Hatavhivyo ameunga mkono kauli ya waziri wa usalama wa ndani Fred matiangi kupiga marufuku disco matanga katika eneo la pwanikwani amesema hatua hiyo itasaidia kupunguza visa hivyo.
Taarifa na Hussein Mdune.