Mwanasiasa wa chama cha ODM mjini Mombasa Mohammed Nyambwe amesema visa vya wahudumu wa bodaboda katika eneo la Likoni kulengwa na wahalifu vitapungua kupitia ushirikiano wa viongozi na idara ya usalama.
Nyembwe amewataja wahudumu wa bodaboda kama watu wanaopitia changamoto nyingi wanapoendeleza biashara yao na wanahitaji kuhakikishiwa usalama.
Aidha Nyembwe amewahimiza wahudumu wa bodaboda eneo hilo kutoa ripoti kwa idara ya usalama wanapokumbana na visa vya uhalifu.
Mwanasiasa huyo amezungumza hayo Likoni alipoongoza hafla ya uzinduzi rasmi wa michuano ya kandanda katika kombe la NYEMBWE CUP.
Taarifa na Hussein Mdune.