Mradi wa studio mashinani ulioanzishwa kwa madhumuni ya kuwasaidia wasani kutoka kanda ya Pwani unatafuta watayarishaji wa mziki.
Kulingana na taarifa kutoka kwa wizara inayoshughulika na mradi huo ni kuwa inalenga kufanya mkutano na watayarishaji wa mziki kutoka Pwani ili kujadiliana kuhusu mambo kadha wa kadha.
Hata hivyo haijabainika iwapo wanatafuta producer wa kumuajiri au la huku duru za kuaminika zikigusia kuwa huenda kunatafutwa mtayarishaji atakayefanya kazi katika studio hizo za serikali.
Watayarishaji wote wa mziki kutoka Pwani wanafaa kufika katika ofisi za mradi huo zilizoko Sauti House mjini Mombasa, siku ya Alhamisi saa mbili asubuhi.