Stivo Simple Boy amefunguka na kusema kwamba ameshawahi kuwekwa korokoroni kwa wiki baada ya rafiki wake wa kike kumshtaki kwa madai ya uongo kwamba amemnajisi.
Akizungumza na kituo kimoja cha habari jijini Nairobi, rapa huyo ameeleza kuwa rafiki alikuwa anamtamani kimapenzi na alizua madai hayo ili kufanya kiki baada ya kumkataa, lakini mamake hakulichukulia kama mzaha na kumuitia maafisa wa polisi.
Aidha, Stivo alichiliwa baada ya majibu ya vipimo vya daktari kuonyesha kwamba msichana huyo alikuwa anadanganya.
Hata hivyo, mwanamuziki huyo bado anashikilia kwamba anafuata sheria za dini na kubaki bikra hadi atakapooa.