Msanii wa Bango aliyejipa jina la First Lady, Stella Mbeyu amebarikiwa na mtoto.
Stella Mbeyu anayevuma na vibao kama vile Father Katana, Darling, na Kama hunitaki niache aliajalia na mtoto huyo siku ya tarehe 7 Machi.
Kupitia kwa ukurasa wake wa Facebook msanii huyo aliutaja ujio wa mwanawe kama wa baraka kubwa kwake.
“Raha isiyo kifani welcome to the world my baby boy Ryan Baya Gunga am so happy sijaamini bado thanks LORD”
Kutoka kwa Uhondo tunamtakia kila la kheri Stella Mbeyu.
Taarifa na Dominick Mwambui.