Picha kwa Hisani –
Tume ya kutathmini mishahara na marupurupu ya wafanyikazi wa umma nchini SRC imezindua awamu ya tatu ya mpango wa kutoa marupurupu kwa wafanyikazi wa umma humu nchini
Katika kikao na wanahabari jijini Nairobi mwenyekiti wa tume hio Lyn Mengich amesema mpango huo utatekelezwa kwa miaka minne kuanzia mwaka 2021 hadi mwaka 2025 na utachukua tume hio miezi kumi kujiandaa kutekeleza.
Mengich amesema tume hio itatathmini upya mishahara yote ya wafanyikazi wa umma ikiwemo ule wa rais ili kufahamu wale wanaostahili kuongezewa ama kupunguziwa mishahara.
Mwenyekiti huyo wa tume ya SRC aidha amesema suala la kuongezwa mishahara kwa wafanyika wafanyakazi wa umma litazingatia bidii miongozi mwa maafisa hao wa umma.