Picha kwa hisani –
Tume ya kutathmini mishahara na marupurupu ya wafanyiakzi wa umma nchini SRC tayari imewasilisha barua kwa rais Uhuru Kenyatta ikimtaka kutotia saini mswada unaolenga kuwalipa shilingi laki moja kwa mwezi wabunge waliohudumu kati ya mwaka 1984 hadi 2001.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari mwenyekiti wa tume hio Lyn Mengich amesema iwapo mswada huo utapitishwa na kuwa sheria utaleta athari kubwa kwa uchumi wa taifa,kwani maafisa wengine waliohudumu serikalino huenda wakataka malipo sawa na hayo.
Mengich amesema tume hio inapinga mswada huo kwani hauangazii usawa ,akisema kuna maafisa wa serikali waliostaafu na wanapitia maisha magumu pasi na kupewa marupurupu yeyote na serikali.
Kauli yake inajiri huku wizara ya fedha nchini ikiweka wazi kwamba huenda malipo hayo yakakosa kutekelezwa ikizingatiwa kwamba bajeti ya kitaifa ya mwaka huu wa kifedha wa 2020/2021 ina mapungufu.