Story by Hussein Mdune-
Mvutano wa kisiasa unaoendelea kushuhudiwa katika bunge la kitaifa kuhusu ni mrengo upi wa kisiasa ulio na idadi kubwa ya wabunge, unatarajiwa kupata ufafanuzi zaidi kutoka kwa Spika wa bunge hilo Moses Wetangula.
Baadhi ya viongozi wa kidini katika kaunti ya Mombasa wakiongozwa na Askofu wa Kanisa la Ushindi Baptist eneo la Likoni Joseph Maisha, wamewataka wabunge kutatua mvutano huo kwa njia ya maelewano.
Askofu Maisha amesema ni jukumu la Spika wa bunge hilo kuzingatia vigezo vya bunge na sheria jinsi inavyoeleza kuhusu swala hilo na kufanya maamuzi ya busara ili kuzuia sintofahamu za kiuongozi.
Siku ya Jumanne wakati wa kikao cha kwanza cha bunge hilo la kitaifa, hoja hiyo ilikosa suluhu baada ya wabunge kutofautiana katika swala hilo huku kila mrengo wa kisiasa hasa Kenya kwanza na Azimio ikiwa tayari wamependeza baadhi ya viongozi kushikilia nafasi za kamati mbalimbali za bunge hilo.