Story by our Correspondents –
Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai amejiuzulu wadhfa wake kutokana na kutofautiana kauli kati yake na Rais wa taifa hilo Samia Suluhu Hassan.
Hatua hiyo ya kujiuzulu kwa Spika Ndugai huenda ikachangia mpasuko ndani ya Chama Cha Mapinduzi CCM kwani inadaiwa kwamba hatua hiyo imechangiwa na shinikizo kutoka kwa wanachama wa CCM kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania kumtaka spika huyo ajiuzulu kutokana na kwenda kinyume na Rais Samia.
Katika barua yake ya kujiuzulu aliyoitoa kwa vyombo vya habari ambayo alimuandikia katibu wa CCM, Spika Ndugai amesema amechukua uamuzi huo kwa hiari.
Siku chache zilizopita Spika Ndugai alionekana kupinga hatua ya Rais Samia ya kuchukua mikopo kutoka mataifa ya ulaya huku akidai kwamba mikopo hiyo itasababisha nchi kupigwa mnada.