Picha kwa hisani –
Spika wa bunge la Nairobi Benson Mutura anatarajiwa kuapishwa muda wowote kuanzia sasa ili kuanza kuhudumu kama kaimu gavana wa kaunti ya Nairobi.
Hafla ya kuapishwa kwake itaandaliwa katika makao makuu ya kaunti ya Nairobi ,na kuapishwa kwake kuchukua nafasi hio kunajiri saa chache baada ya aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko kubanduliwa mamlakani kwa makosa mbali mbali.
Mutura aliwahi kuhudumu kama mbunge wa makadara ndani ya kaunti ya Nairobi, kabla kuchaguliwa kwake kuwa spika wa bunge la Nairobi mapema mwezi agosti mwaka huu,baada ya aliyekuwa spika wa bunge hilo Beatrice Elachi kujiuzulu.
Itakumbukwa kwamba sonko alivuliwa mamlaka hapo jana baada ya masenta 27 kati ya maseneta 47 kuunga mkono hoja ya kubanduliwa kwake.