Story Rasi Mangale-
Spika wa bunge la kaunti ya Kwale Sammy Ruwa amesema bunge hilo limetekeleza majukumu yake vyema chini ya uongozi wake hasa kwa kuzingatia kanuni za katiba.
Katika kikao na Wanahabari, Ruwa ambaye amejitosa katika kinyang’anyiro cha kuwania ugavana wa Kwale, amesema bunge hilo limetambua mahitaji ya wananchi na kupitisha miswada mbalimbali iliyomlenga mwananchi
Ruwa ameahidi kuhakikisha anapigania kikamilifu haki za wakaazi wa kaunti hiyo kwa kuhakikisha miradi ya maendeleo inaidhinishwa mashinani sawa na kulishinikiza bunge hilo kupitisha mswada itayomfaidi mwananchi iwapo atachaguliwa kuwa gavana wa kaunti ya Kwale.
Wakati uo huo amesema ni jukumu la serikali ya kaunti ya Kwale chini ya uongozi wa Gavana wa sasa wa Kwale Salim Mvurya kuonyesha kwa wananchi miradi ya maendeleo aliyoidhinisha katika kipindi chake cha uongozi na wala sio kuwakosoa wengine.
Kauli yake imejiri huku Gavana wa Kwale Salim Mvurya akitarajiwa kulihutubia bunge la kaunti hiyo siku ya Jumatano sawa na kuwalisilisha ripoti ya utendakazi wa serikali yake bungeni humo.