Story by Rasi Mangale–
Mgombea huru wa kiti cha ugavana wa kaunti ya Kwale Sammy Ruwa, ameleezea kuridhishwa kwake na zoezi la upigaji kura linaoendeshwa na tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC.
Akizungumza na Wanahabari baada ya kupiga kura katika kituo cha kupigia kura katika shule ya upili ya Mwereni eneo bunge la Lungalunga kaunti ya Kwale, Ruwa amesema zoezi hilo linaendeshwa vyema na maafisa wa IEBC.
Ruwa aidha wamewahimiza wananchi katika kaunti hiyo kujitokeza kwa wingi na kutekeleza jukumu lao la kikatiba la kupiga kura.
Wakati huo uo amewahimiza wananchi kuzidi kudumisha amani wakati huu wa uchaguzi mkuu ili zoezi la upigaji kura lifanyike kwa amani.