Story by Our Correspondents –
Spika wa bunge la kitaifa Justin Muturi ameipa siku 14 kamati ya bunge la kitaifa kuhusu fedha chini ya Mwenyekiti wakeGladys Wangakuchaguzi swala la nyongeza ya bei za bidhaa za petroli nchini na kuwasilisha ripoti bungeni.
Spika Muturi amesema baada ya kamati hiyo kuwasilisha ripoti bungeni ndipo bunge litabaini jinsi litakavyoshughulikia swala hilo tata ili wakenya wapate afuani kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha.
Hata hivyo kabla ya Spika kutoa agizo hilo, wabunge wameikashfu vikali serikali, Wizara ya madini na petroli nchini, Mamkala ya KRA na ile ya EPRA kwa kuongeza bei za bidhaa za petroli nchini huku nchi jirani zikiweka bei wastani kwa wananchi wao.
Hata hivyo ombi la kufanyia marekebisho bei ya bidhaa za mafuta nchini ili kuhakikisha wakenya wanamudu gharama ya maisha limewalishwa mbele ya Spika Muturi na Anthony Manyara na John Wangai.