Story by Our Correspondents-
Bodi ya uchaguzi ya chama cha WIPER imeweka wazi kwamba aliyekuwa wakati mmoja Gavana wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko atajitosa katika kura za mchujo wa chama hicho kuwania tiketi ya kugombea ugavana wa Mombasa.
Naibu Mwenyekiti wa Bodi hiyo Agatha Solitei, amesema Sonko atashiriki zoezi la kura ya mchujo ya chama hicho ambapo atamenyana na Mbunge wa Kisauni Ali Mbogo anayelenga kupeperusha bendera ya chama hicho kuwania kiti cha ugavana wa Mombasa.
Solitei amesema jina la Sonko tayari limewasilishwa na chama hicho kwa Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC kwamba ni kati ya wagombea wanaolenga kutafuta tiketi ya chama hicho ili kuwania kiti cha ugavana wa Mombasa.
Sonko anajumuisha idadi ya wanaowania kiti cha ugavana wa Mombasa kuwa watu watano, akiwemo Mfanyibiashara na mwanasiasa Suleiman Shahbal, Abdulswamad Sharrif Nassir, Ali Mbogo, Mike Mbuvi Sonko, na Antony Chitavi.