Story by Our Correspondents-
Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC imesema haitamuidhinisha mgombea wa kiti cha ugavana wa kaunti ya Mombasa kwa tiketi ya chama cha Wiper Mike Mbuvi Sonko.
Mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati, amesema Sonko pamoja wenzake wawili wanakabiliwa na kesi za ukosefu wa uadilifu ndiposa wakatimuliwa mamlaka kwa utumizi mbaya wa afisi za umma.
Kwenye kikao na Wanahabari katika ukumbi wa Bomas jijini Nairobi, Chebukati amesema kwa kuzingatia kifungu cha sita cha Katiba kipengele cha 75 kuhusu uongozi na uadilifu Sonko hawezi kuidhinishwa na tume hiyo kuwania ugavana wa Mombasa.
Kauli ya Chebukati imejiri baada ya Tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini EACC kuwasilisha orodha ya majina 241 kwa IEBC ya viongozi ambao wanakabiliwa na kesi mbalimbali mahakamani ili wazuiliwe kuwania nyadhfa za uongozi nchini.