Gavana wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko ameteua Ann Kananu Mwenda kuwa naibu Gavana wa kaunti ya Nairobi, ikiwa ni miaka miwili sasa tangu aliyekua Naibu gavana kaunti hiyo Polycarp Igathe kujiuzulu.
Gavana sonko amesema Bi Kananu ataanza rasmi kutekeleza majukumu yake punde tu wawakilishi wadi wa bunge la kaunti ya Nairobi watakapokamilisha zoezi la kumpiga msasa.
Sonko amewataka wajumbe wa bunge la kaunti ya Nairobi kuharakisha zoezi la kumpiga msasa Bi Kananu ambae kwa sasa anahudumu kama afisa mkuu wa kitengo cha kukabiliana na majanga.