Gavana wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko kupitia kwa kitengo cha Sonko Rescue team kimempeleka bondia Conjestina Achieng hospitalini.
Sonko amechukua hatua hiyo baada ya video ya Conje kuzagaa mtandaoni ambapo alikuwa anaonekana kudhoofika kiafya.
Kupitia kwa ujumbe aliouweka katika mtandao wa kijamii Sonko amesema kuwa baada ya kumpa Conjestina matibabu atamtafutia ajira.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo mchezaji wa zamani wa timu ya taifa Harambee Stars Musa Otieno ameiotolea wito serikali kuu kuwasaidia wanamichezo wengine wakongwe ambao hali zao zinazidi kudhoofika.
Kulingana na Otieno aliyeichezea Harambee Stars kati ya mwaka 1993- 2009 ni kuwa wanamichezo wengi wameacha katika hali ya uchochole licha ya kuiletea Kenya sifa tele.
Conjestina anasumbuliwa na matatizo ya kiakili hali iliyomfanya kusambaratika.
Taarifa na Dominick Mwambui.