Picha kwa hisani –
Aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko amefikikishwa katika mahakama ya Kiambu kujibu mashtaka 12 yanayomkabili aliyoyatekeleza kati ya mwaka 2019 hadi mwaka huu wa 2021 ikiwemo wizi wa mabavu na uchochezi wa ghasia.
Kabla ya kuwasilishwa mahakamani Sonko amepelekwa mbele ya makachero wa idara ya upelelezi wa jinai DCI kuandikisha taarifa baada ya katibu katika wizara ya usalama wa ndani Dkt Karanja Kibicho kuwasilisha kesi dhidi yake kwamba amemuharibia jina.
Hata hivyo mawakili wa Sonko wakiongozwa na John Khaminwa wamewasilisha hoja ya usalama wa mashahidi wakisema wana ushahidi wa kutosha kutetea mteja wao na kwamba lazima mashahidi wao wapewe ulinzi mkali.
Hapo jana sonko alihojiwa na maafisa wa idara ya DCI kuanzia saa kumi jioni hadi saa nne usiku na kupelekwa katika kituo cha polisi cha Muthaiga na kuzuiliwa usiku mzima.