Picha kwa hisani –
Aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko amelazwa katika hospitali moja jijini Nairobi baada ya kukumbwa na matatizo ya tumbo.
Kulingana na wasaidizi wake,Sonko ambae amekua akizuiliwa katika kituo cha polisi cha Gigiri alitarajiwa kuwasilishwa mahakamani hii leo kujua hatima yake iwapo ataachiliwa kwa dhamana,na kwamba hali yake ya kiafya imeimarika.
Sonko anatarajiwa kuwasilishwa katika mahakama ya Kiambu kujua uamuzi wa ombi alililowasilisha na kuachiliwa kwa dhamana kwenye mashataka zaidi ya kumi na mbili yanayomkabili ikiwemo wizi wa mabavu na uharibifu wa mali.
Mahakama ya Kahawa magharibi pia ilitarajiwa kutoa uamuzi wa ombi la maafisa wa idara ya DCI la kutaka sonko azuiliwe kwa siku 30 ili kukamilisha uchunguzi wao kuhusu madai ya ugaidi yanayomkabili mwanasiasa huyo.