Mwanamuziki size 8 amuteka mtandao wa kijamii baada ya kufichua amekuwa akikumbana na changamoto za kiafya kwa kipindi cha miaka mitano.
Mama huyo wa mtoto mmoja amekuwa akikariri kuwa kuzaliwa kwa mwanawe ilikuwa ni miujuza ambayo ana mrejeshea Mungu shukurani.
Jambo ambalo watu wengi wasilofahamu ni kuwa tangu kuzaliwa kwa mwanawe, mwimbaji huyo amekuwa hospitalini kila mara kwa sababu ya kusumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu.
Kupitia kwa ujumbe mfupi aliyoweka kwenye mtandao wake wa Instagram, mama huyo aliandika kuwa licha ya kuwa maisha yake yamo mikononi mwake, bado anashukuru kuwa hai.
Size 8 ambaye alikuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kutimiza miaka 32, alimuomba Maulana kumubariki katika miaka zijazo na pia kwa kuwakinga wanawe watarajiwa huku akiendelea kukumbana na maisha haya magumu.