Msanii Dogo Richie amesema kuwa hana tatizo na wimbo wa Lava Lava ambao umeonekena kuiga wimbo wake.
Msanii Lava Lava kutoka label ya Wasafi aliachilia wimbo kwa jina Go Gaga ambao umeonekana kuiga ule wa Dogo Richie ulio na kichwa sawa.
“Sijauzia Wasafi wazo la wimbo huu wala sina tatizo na LavaLava kuhusiana na wimbo wake mpya. Mawazo ya wasanii husawiana wakati mwingine,” amesema Dogo Richie.
Msanii huyo aidha ameongezea kuwa mziki kutoka Pwani umekua na unasoko kubwa ikilinganishwa na zamani.
“Mziki wetu kwa sasa ni tofauti sana na kitambo, unapenya katika soka la Afrika. Ngoma ya Lava Lava ni dalili kuwa tunasikilizwa sana Tanzania na wasanii wa huko pia wanatukubali,” ameongezea msanii huyo.
Taarifa na Dominick Mwambui.